Maneno ya Wema Kabla ya Lema Kuhutubia Arusha Leo


MSANII wa filamu na malkia wa mtandao nchini Wema Sepetu ‘Madam’,  amejikita zaidi katika siasa baada ya kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivi karibuni.


Wema ameendelea kuzianika mitandaoni  baadhi ya harakati zake za kisiasa ikiwa ni pamoja na kujihusisha na shughuli za kijamii kama vile upandaji wa miti,  uliofanywa na baadhi ya viongozi wa chama hicho na leo kabla ya Lema kuhutubia, ameweka picha na ujumbe mtandaoni unaowahamasisha watu kufika katika mkutano huo.


“All Ready Kwa Ajili ya Mkutano wa Mhe. GodBless Lema… See you there…. Giving MY Chadema A New Look… Y’all Know Black And Khaki Be our Colour…. A lil White to add Flavor wont Hurt Nobody…. #CallMeKamanda cc @upendosimwita1 @_elm_ @blowassa”, alimaliza Wema.