Showing posts with label WASANII. Show all posts
Showing posts with label WASANII. Show all posts

HUSSEIN Machozi - Italy Hajulikani Alikiba Wala Diamond..!!!

Msanii wa muziki, Hussein Machozi, amefunguka kwa kudai kuwa hakuna msanii wa muziki kutoka Tanzania ambaye anajulikana nchini Italy.
Aidha amedai muimbaji kutoka Kenya, Stella Mwangi ambaye anaishi nchini Norway ndiye msanii wa Afrika Mashariki anayefanya vizuri.
Muimbaji huyo aliyewasili nchini Tanzania wiki hii akitokea Italy, amedai nchini Italy muziki wa Tanzania haujafika na hata wasanii wanaofanya vizuri nchini kwa sasa akiwemo Diamond na Alikiba hawajulikani.
“Hapana lakini kuna mtu mmoja alishaniambia kuhusu msanii wa Kenya anaitwa Stella Mwangi wanamfahamu fahamu, siyo kivile sana kutoka East Africa,” alisema Hussein.
Aliongeza, “Bongo Fleva Italy sijawahi kuisikia kiukweli wa Mungu. Kama kuna mshikaji mmoja nilimwambia kwetu kuna msanii mkali sana anaitwa Diamond nikawa nimempa link akawa shabiki, akawapa na wengine wakawa mashabiki wa Diamond kinyama.,”
Muimbaji huyo amedai amekuja nchini kwaajili ya kuachia kazi zake mpya za muziki na baada ya hapo atarejea tena Italy kwaajili ya kuendelea na masom
Mbwana Samatta Atoa ya Moyoni Baada ya Makonda Kuvamia Clouds Usiku Usiku Akiwa na Kikosi cha Askari..!!!
BAADA ya kuvamiwa kwa Kituo cha Redio cha Clouds Fm, imeibuka mijadala mingi, Watanzania wakaijadili kila kona ya nchi. Katika mijadala hiyo, wapo wanasiasa, watumishi wa umma, waumini wa dini na wanamichezo ambapo mchezaji wa Taifa Stars anayekipiga nchini Ubelgiji katika Klabu ya Genk, Mbwana Samatta amefunguka kuwa wanasiasa wanakosa maadili.
“Ndiyo maana siasa imekuwa cheap maana viongozi wenyewe wana-hang out na akina Amber Lulu na Gigy Money” aliandika Samatta.
Credit -Globalpublisher
Afande Sele Amfananisha Bashite na Tumbili Aliyemaliza Kurukia Miti yote na Sasa Ameamua Kumrikia Anayemfuga...
Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva Mwana Hip Hop Afande Sele TheKing ametoa ya moyoni baada ya Kuibuka Tetesi za Uvamizi wa Clouds Media.Kupitia Ukurasa wake wa Facebook Msanii huyo ambaye ndie mfalme wa kwanza wa Miondoko ya Kufokafoka nchini ameandika ya fuatayo:-
“Kama ni kweli Bashite ameongoza watu kufanya uvamizi kwenye kituo cha clouds media kwa jinsi inavyojieleza…Basi atakua mfano wa tumbili aliyemaliza kurukia miti yote sasa ameamua kurukia mwili wa anaemfuga…Na’Anko’akiendelea kushupaza shingo ktk hili huenda yale maandiko yakatimia kabla ya muda tarajiwa…muwe na Jpili Kareem akina ndugu…..” – Afande sele aliandika kupitia akaunti yake ya Facebook.
Hii hapa Original Post.
“Kama ni kweli Bashite ameongoza watu kufanya uvamizi kwenye kituo cha clouds media kwa jinsi inavyojieleza…Basi atakua mfano wa tumbili aliyemaliza kurukia miti yote sasa ameamua kurukia mwili wa anaemfuga…Na’Anko’akiendelea kushupaza shingo ktk hili huenda yale maandiko yakatimia kabla ya muda tarajiwa…muwe na Jpili Kareem akina ndugu…..” – Afande sele aliandika kupitia akaunti yake ya Facebook.
Hii hapa Original Post.
Subscribe to:
Posts (Atom)