Diva Love Afunguka 'Ningekuwa Mwanaume Ningetoka na Jokate Kimapenzi'

Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM Diva amesema kama angekuwa ni Mwanaume angem’date Jokate kwani anavutiwa sana na muonekano wake wa baby face,pia amekiri kuwa alishawahi kumchangia Charity yake.

Mbali na hilo Diva amefunguka na kusema kuwa hawezi kumuomba msamaha Jokate Mwegelo ingawaje yeye alishawahi kumuona mrembo huyo akimrushia maneno kwenye mitandao ya kijamii.
.
.
. “Siwezi kumuomba msamaha Jokate kwa sababu sijamkosea chochote kama yeye alinikosea aje yeye kuniomba msamaha“Alisema Diva

Miezi kadhaa iliyopita @Divathebawse aliwahi kumtaka Alikiba aachane na @Jokatemwegelo akidai kuwa mwanadada Huyo ndio anamtia gundu king wa bongo fleva