Jamani Nitoke Nnje ya Ndoa..?Nahitaji Ushauri Wenu...!!!


Nimevumilia majaribu ya ndoa yamenishinda, ninaishi na mke wangu lakini hatuna furaha yaani kama tumelazimishwa! 

Hakuna kabisa furaha, tumejaribu kukaa chini na kujadili mara nyingi sana lakini huwa anadai hakuna tatizo! Najiuliza sana hivi kutoka nje ya ndoa kutanosaidia nini? Nitachinwa pesa bure na ndo matatizo yataongezeka lakini pia kiimani hairuhusiwi nami naogopa kukutwa katika dhambi na Mungu wangu!

Nimesali sana lakini kama hakuna badiliko lolote! Nimuache? Yaani kila kitu tabu tupu! Wasichana nawaogopa mno nahisi wataniongeza machungu je, nitamfute mmama wa wastani kama miaka 34 ila awe mzuri? mi nina 25. Kwakweli sijitambui niko njia panda!

Nilikuwa mwajiriwa wa kampuni fulani na nilikuwa nikilipwa laki 5 kwa mwezi sasa nina miezi 2 nkmeacha kazi sababu ya matatizo ya ndoa yangu!

Sijielewi nahisi naelekea kufa ningepata mwanamke wa umri huo na anaishi tofauti na.mji wangu na akanipenda ningeenda kukaa kwake hata kwa miezi 3.
Nahisi maisha yangu yanaharibika sasa,

Nina uchungu sana usiku huu nilikuwa safari nimerudi na zawadi zimepokelewa na kutupwa sitting rum, ninahamu nimemsogelea kitandani kanipiga pepisi jichoni nomeumia sana maana tangu tuoane sijawahi ifurahia ndoa!

Hapa najiuliza nifanyeje napanga nitoke nikalale guest lakini sina hata wakunifariji natoka naenda guest hata nikifika nikaamua kujitoa duniani inatosha.

Kuna wanawake wazuri sana, wapoleee sauti za upole akikukosea kidogo tu utasikia samahani baba yangu, nakupenda haikuwa nia yangu, jaman namimi si nipate mmoja wa hivi?