Zile tetesi za Msanii Tiwa savage kutoka Nigeria kusainiwa katika label ya Roc Nation ya Rapper Jay Z zaweza kuwa sio tetesi tena, hiyo inatokana na Tiwa Savage pamoja na Manager wake Don Jazzy wa Mavin Record kupost katika kurasa zao za Instagram, picha inayoashiria kama ule mpango wa kusaini umetimia.
Hii imetokea siku chache baada ya Rapper Wale kusema alishawahi kumpendekezaWizkid kusainiwa kwenye record label ya Roc Nation katika moja ya Interviews alizowahi kuzifanya.
Kama kweli Tiwa Savage atakuwa amesaini Roc Nation atakuwa ni msanii wa kwanza wa kike kutoka Africa kusainiwa chini ya record label hiyo kwani yupo Rapper Wale ambaye ni Raia wa Marekani lakini ana asili ya Nigeria.