GoodNews: A.K.A wa South Africa kapata dili la kuperform main Stage ya BET

Tuzo za BET ni tuzo kubwa za muziki kutoka Marekani na zenye heshima kubwa duniani, ambapo mwaka huu zitafanyika June 26 2016 Los Angeles Marekani. Kama kawaida wasanii wataperform ila good news ni kutoka kwa rapper A.K.A kutoka South Africa ambaye nae anaingia katika histori ya msanii wa Afrika kupata nafasi ya kuperform kwenye main stage.
AKA
Sambamba na A.K.A wasanii wengine watakaofanya perfomance siku hiyo ni pamoja na Rapper Fat Joe, Lil Wayne ,2chainz, Fetty WapDesiigner na wengine wengi. A.K.Aatakuwa msanii wa kwanza kutoka Africa kuperform kwenye Main stage ya tuzo za BET ikiwa inaashiria kiasi gani muziki wa Africa unazidi kufanya vizuri duniani.
AKA
A.K.A atafanya show kwenye  tuzo za BET June 25 2016,yaani siku moja kabla ya tuzo zenyewe kufanyika katika ukumbi wa Microsoft Theater, hii ni good news nyingine kwa muziki wa Afrika baada ya siku chache Chris Brown kumualika Wizkid katika tour ya ONE HELL OF A NIGHT TOUR.
  KAMA ULIIKOSA SHOW YA MIAKA 10 YA CHRISTIAN BELLA