Bajeti ya serikali ya Tanzania ilisomwa June 8 2016 na ikawa gumzo kwenye vitu mbalimbali ambavyo kodi yake imepanda vikiwemo vinywaji baridi, vinywaji vikali pamoja na namba binafsi za magari.
Namba binafsi za magari ambazo watu wengi wameweka majina yao akiwemo staa wa bongofleva Diamond Platnumz ambapo mwanzoni ada yake ilikua ni milioni 5 kwa miaka mitatu ila sasa hivi ni milioni 10 kwa miaka mitatu.
Time hii ya bajeti ya Tanzania imeenda sambamba na bajeti za nchi nyingine za Afrika Mashariki za Rwanda na Uganda pia ambapo Uganda wamepandisha pia ada za namba binafsi za magari kutoka shilingi milioni 5 ya awali mpaka shilingi milioni 20 za Uganda ambazo zinacheza kwenye milioni 13 za Tanzania.