Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mwanamuziki Vanessa Mdee maarufu Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.Vanessa ni miongoni mwa watu waliotajwa katika orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya, lakini hakuweza kuripoti kwa wakati sababu alikuwa nchini Afrika Kusini kikazi.
Baada ya kujisalimisha, Jeshi la Polisi lilifanya upekuzi nyumbani kwake kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wwa Serikali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Jeshi la Polisi hadi sasa halijatoa taarifa kuhusu tukio hilo na kama walikuta ushahidi wowote nyumbani kwa mwanamuziki huyo.