Imevuja! Siri ya maisha mazuri ya baadhi ya mastaa wa kike Bongo ambao hawafanyi filamu, Bongo Fleva wala kazi yoyote imejulikana huku aibu kubwa ikiwafuata nyuma ya siri hiyo, Risasi Jumamosi limefungasha mzigo wa kutosha!
Kwa mujibu wa chanzo chetu kikuu kikizungumza na Risasi Jumamosi, mastaa hao wamekuwa wakitumia njia ya kisasa ambayo ni Mtandao wa Kijamii wa Instagram kupata wanaume wenye fedha ambao hujitokeza na kuwataka kimapenzi, wengi wao wakiwa nje ya nchi.
Giggy Money
NCHI ZENYE WATEJA WENGI
Chanzo hicho ambacho na chenyewe ni staa, kiliendelea kusema kuwa, nchi ambazo mastaa hao wana soko kubwa ni China, Dubai na Afrika Kusini. India ni kwa mbali sana!
INAVYOKUWA SASA
Chanzo: “Ili tuweze kuonwa na wateja wetu hao, huwa tunatupia kwenye mtandao huo, picha zetu zenye mvuto tukiwa kwenye mapozi ya ‘ki-hasarahasara’, wengine hutupia mpaka picha za nusu utupu ili wanaume wakiwaona wavutike haraka.
“Baada ya wanaume wateja kuziona picha zetu kwenye Instagram na kuvutiwa, sasa hutaka kuwasiliana kwa kutumia Insta Direct (mawasiliano ya wawili tu ‘in box’).
“Hapo sasa ndiyo huwa pazuri, kwani kama mwanaume atakuwa amekolea, atatangaza dau na kumtaka staa aliyempenda amfuate nchini mwake. Kama ni Dubai, China au Afrika Kusini,” kilisema chanzo hicho.
Kidoa
UJIRA WAO
Chanzo hicho kilisema kuwa, ujira wanaolipwa mastaa hao ni wa chini sana ukilinganisha na kiwango cha muda.“Mara nyingi kama ni Dubai, unatangaziwa dola za Marekani 3,000 (kama shilingi milioni 6) ambapo ndani ya humo ni pamoja na tiketi yako ya ndege kwenda na kurudi, malazi ya kule kwa maana ya kukaa hotelini na kula.
“Siku ukirudi unapewa labda dola 500 tu ambazo ni kama shilingi milioni moja na kidogo. Sasa hizo, ndiyo utaingia madukani kufanya manunuzi mbalimbali ya vitu kama pafyumu, losheni, nguo na viatu. Ndiyo maana masta wengi wakienda nje ya nchi kwa wanaume hurudi na mabegi ya vitu walivyonunua.” Chanzo.
Jackline Wolper
HUWA WANAJAZA NAFASI
Katika hali ambayo ilishtua, staa huyo alisema kuwa, kwa tabia hiyo ya kujiuza nchi mbalimbali, baadhi ya mastaa hujikuta nafasi zimejaa!
“Utakuta staa anatakiwa kwenda Dubai mwezi huu. Mwezi ujao anakwenda China kwa mwanaume mwingine, akitoka China, Afrika Kusini mwezi Aprili. Akitokea mwanaume akamtaka aende Dubai anakuta nafasi imejaa. Pengine mpaka Mei.
“Mkifuatilia sana mtagundua ni kwa nini baadhi ya yetu hatutulii nyumbani Bongo wakati hatuna biashara kusema ndiyo inatufanya tusafiri kila wakati. Ni kujiuza tu! Mh! Mbona Instagram ina mambo!”
SIFA ZAO
“Tena nataka kukuongezea kwamba, ogopa sana mastaa ambao picha zao kwenye Instagram ni za nusu utupu! Hebu we fikiria, Instagram mimi sioni kama ni sehemu ya siri, sasa kwa nini mtu apige picha chafu halafu azitupie kule, anatafuta nini? Maana hata baba yako, mama yako, ndugu zako wanaweza kuona,” alisema staa huyo.
MASOGANGE ALITAJWA
Madai hayo yananyemeleana kwa karibu na habari iliyowahi kuandikwa na Gazeti la Ijumaa la Januari 23, 2015 ikiwa na kichwa kisemacho;
MASOGANGE AIBU TUPU SAUZI
Habari hiyo ilimhusu modo aliyetikisa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’.
Habari hiyo ilisema Masogange yupoyupo tu, kazi kujipiga picha za utupu na kuzitupia mtandaoni kana kwamba anatafuta wanaume.
“Kimsingi hana kazi huku Sauz zaidi ya kuposti picha kwenye Mtandao wa Instagram na anachanganya sana wanaume wenye pesa zao. Si unajua tena mtoto kajaliwa shepu la maana. Ukitaka kuthibitisha hilo ingia katika akaunti yake utaona picha kibao za kihasara akiwa hotelini.”
Hata hivyo, staa huyo alikuja kukanusha kuhusu picha zake na kujiuza huko bondeni ambapo alisema:
“Mie sijui hizo picha zilisambaa vipi sababu zilikuwepo kwenye kamera yangu na mimi siku hiyo nilikuwa nimelewa. Sikuwa naelewa chochote na nilikuwa South Africa (Afrika Kusini). Kwa hiyo masuala ya kuandikwa kwamba nilikwenda kujiuza si kweli.”
KIDOA HIVI KARIBUNI
Hivi karibuni, video queen wa Bongo anayekuja kwa kasi, Asha Salum ‘Kidoa’ naye alisafiri kwenda Dubai akisema amepata dili. Lakini hakuweka wazi ni dili gani kiasi kwamba, katika toleo moja la gazeti ndugu na hili, Ijumaa liliandikwa makala yenye kichwa kisemacho; Kidoa; Dubai umeenda kula bata, kujiuza au dili za ‘sembe’? Katika makala hayo, mwandishi alitilia shaka baada ya kuona picha kwenye Instagram yake zikimuonesha msanii huyo akiwa Dubai akila bata kwenye klabu ya hoteli kubwa.
Wengi baada ya kuona binti huyo yuko Dubai walianza kujiuliza maswali mengi. Kwamba kaenda kujipumzisha na kula bata au kaenda kujiuza kama ambavyo baadhi ya mastaa wamekuwa wakifanya au ameanza kutumika katika kusafirisha ‘sembe’? yaani unga au madawa ya kulevya.
Mwandishi alisema anaandika hayo kwa sababu anajua Kidoa hana mkwanja wa kusema anakwenda kupumzisha akili Dubai.
WENGINE HUWAUZA WENZAO
Katika maelezo mengine ya staa huyo, baadhi ya mastaa hao wanapokuwa nje ya nchi na wanaume wao wa kwenye Instagram hugeuka na kuwa mawakala wa kuwauza wengine.
“Lakini pia staa anaweza kuwa mfano, Dubai halafu akakutana na staa mwenzake anakwenda mfano China, na yeye anakuwa wakala. Mimi niliwahi kukutana na staa mmoja Dubai, anakwenda China, nikampa namba za simu za mwanaume niliyewahi kuwa naye kule.
“Alipofika alimpigia, akamwambia amepewa namba na mimi, basi na mimi nikalipwa changu maana nimemtafutia soko,” alisema staa huyo.