Tundu Lissu Awekwa Rumande Kwa Kukosa Dhamana.



MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana, mara baada ya mahojiano na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kufuatia kauli yake aliyoitoa jana inayoelezwa kuwa si ya kiungwana.

Mbunge huyo amehojiwa kwa saa tatu  kuhusiana na maneno mengine ambayo anadaiwa kuyaandika kupitia mitandao ya kijamii kuwa ni ya uchochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekiri kuwa Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana na hataachiwa leo, hivyo atalala huko mpaka kesho.

Hii ndo kauli iliyomfanya alale rumande