Mimi Sijaumbwa kwa Ajili ya Kuchezea Wanawake – Harmonize
Mkali wa wimbo ‘Bado’ kutoka WCB, Harmonize amesema hana tabia ya kuchezea wanawake hivyo kama wakikubaliana na mpenzi wake wa sasa Jacqueline Wolper watafunga ndoa.
Wolper
Muimbaji huyo ambaye ametoka katika familia ya dini ya kiislamu, ameiambia Bongo5 kuwa dini yake hamruhusu kuwachezea watoto wa kike.
“Kwa sasa kuweka wazi kama tunakaa pamoja au hatukia siyo kitu kizuri cha kuzungumzia kwa sasa,” alisema Harmonize. “Insha’Allah panapo majaliwa tutakaa pamoja kwa sababu mimi sijaumbwa kwa ajili ya kuchezea wanawake,”
Aliongeza, “Nikiwa na mwanamke tunaandaa future, tunakubaliana tukae pamoja, kwa nini tusikae pamoja wakati dini yangu hainkruhusu,”
Harmonize amewataka mashabiki wa muziki wake kutulia kwani kuna mambo mazuri yanakuja.