MAAJABU: Bawa Kubwa la Ndege Laokotwa Kisiwani Pemba..Wataalamu Waanza Kulichunguza

Bawa kubwa la ndege limeokotwa na wananchi jana katika Bahari ya Hindi kwenye Kisiwa cha Kojani, Pemba. Haijafahamika ni la ndege ya shirika gani.

Sehemu ambayo inaaminika ni mabaki ya ndege imevuliwa katika bahari ya hindi katika ufukwe wa kisiwa cha kojani pemba.

Bawa la ndege lililopatikana katika bahari ya kisiwa kidogo cha kojani huko kisiwani pemba zanzibar, yamezusha mjadala mkubwa miongoni mwa wakazi wa kisiwa hicho huku wengi wakiamini ni bawa la ndege ya malaysia ambayo ilipotea bila kujuilikana hatima yake. Ndege ya shirika la Malaysia Airlines yenye chapa MH370, iliotoweka Machi 8 mwaka 2014 haijawahi onekana hadi leo.

Ingawa bado hakuna uhakika ni mabaki ya ndege gani, wataalamu wa usafiri wa anga wamenza hatua ya awali ya uchunguzi wa mabaki hayo ya ndege.

Taarifa zinasema tayari maofisa wa usalama wameanza kulifanyia uchunguzi bawa hilo na huenda si muda mrefu tukapata maelezo ya kutosha kutoka vyombo vinavyohusika