KUFUATIA staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, Helga wiki iliyopita, swahiba wake mkubwa, Ambwene Yessaya ‘AY’ amefunguka kuwa naye yuko njiani. Akizungumza na mtandao huu, AY anayebamba na Ngoma ya Zigo alisema kuwa ni jambo jema kwa rafiki na ndugu yake wa karibu (MwanaFA) kufunga ndoa hivyo imempa hamasa.
“Nimefurahi sana kwa swahiba wangu kufunga ndoa. Naamini FA amefungua ukurasa mpya katika maisha yake ya kuwa na mwenzake. Nami nipo njiani kumfuata Mungu akipenda,” alisema AY bila kumuweka wazi mwandani wake anayetarajia kufunga naye ndoa.