Showing posts with label MITINDO. Show all posts
Showing posts with label MITINDO. Show all posts

JE UNAMFAHAMU MISS TANZANIA HALALI WA MWAKA 2014/2015,TUMEKUWEKEA HAPA PICHA ZAKE(S3XY),NA TAARIFA ZAKE,,SIO SITI!!

Aliyekuwa mshindi wa pili kwenye shindano la Miss Tanzania 2014, Lillian Kamazima amekabidhiwa taji la Miss Tanzania 2014 na kamati ya Miss Tanzania baada ya Sitti Mtemvu kujivua.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam, Lilian ameahidi kuisadia jamii ya Tanzania.

Nashukuru kupata nafasi hii, naitwa Lillian Kamazima nina miaka 18, nitatumia nafasi hii kusaidia jamii nikishirikiana na kamati ya Miss Tanzania na pia kuiwakilisha Tanzania katika Miss World
alisema Lilian. Lilian ni mrembo kutoka Arusha.

JE ULISOMA HII,,Waganda Wacharuka Mitandaoni na Kusema Miss wao Mpya ni Mbaya Hakustahili Kushinda!!!

Waganda katika mitandao ya kijamii wamecharuka na kuwakaba koo waandaaji wa Miss Uganda kuwa mshindi aliyepatikana Leah Kalanguka Miss Uganda 2014 ni mbaya na hakufaa kushinda taji hilo.

Kwa kumuangalia tu mrembo huyu, ni kweli hakustahili taji hilo?

HUU NI UKAHABA UNAOFANYWA NA WADADA HUKO FACEBOOK!! WAME ZA WATU KUWENI MAKINI!!


Siku hizi wadada kuonyesha makalio yao imekuwa Dili sana tena wengine wamefanya kuwa kama ni Biashara zao za kuwaignizia kipato. sasa huyu Dada c anatafuta Mabwana za watu. ndo nini kupost Picha kama Hizi katika Wall yake katika mitandao ya kijamii?? kama sio ukahaba ni kitu gani. Tena nyie wanaume kuweni makini sana na mitandao hii maana wengi hufanya hizi ili kuwakamata watu wengi hasa mabwana za watu. kama uliwahi kusikia kwamba dada mmoja laiyekuwa akiwaambukiza watu ukimwi kwa makusudi, tena kupitia mitandao hihi ya kijamii!! Kumbuka sio kila king'aacho ni Dhahabu" pia MICHEPUKO SIO DILI BAKI NJIA KUU"

VYAKULA VINAVYOONGOZA KUONGEZA AKILI KWENYE UBONGO


BILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaoutilia maanani. Ubongo ndiyo kiungo kinachohusika na utendaji kazi wote wa mwili na ndiyo unaowezesha mwili kuishi maisha ya furaha au karaha.
Hata hivyo, wakati mwingine utendaji kazi wa mwili unaweza kuwa siyo mzuri kutokana na sababu mbalimbali zinazoathiri ubongo, mojawapo ikiwa ni kukosekana kwa lishe bora na staili ya maisha inayotakiwa kuimarisha ufanisi wa ubongo.
Chakula ni moja ya sababu za msingi kabisa za kuimarisha ufanisi wa ubongo na kuzuia magonjwa mengine ya akili. Lakini kwa bahati mbaya watu wengi hawajui wale vyakula gani kwa lengo la kujenga akili na kuimarisha ubongo.
Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:
MAFUTA YA SAMAKI
Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.
PILIPILI KALI
Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.
MBEGU ZA MABOGA
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, inakuwa poa.
NYANYA
Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.
BROKOLI
Brokoli ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee.
KARANGA
Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.
MAYAI
Mwisho ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.