Showing posts with label MBIO ZA URAISI. Show all posts
Showing posts with label MBIO ZA URAISI. Show all posts

Maneno 36 ya Waziri Membe Kuhusu Mtu Aliyekamatwa na Mabilioni ya Wajumbe Dodoma..

Kuna stori zimeenea mitandaoni kwamba kuna mtu ambae amekamatwa na mabilioni ya pesa Dodoma, kingine ni kwamba amekamatwa na simu ikiwa na maelekezo kwamba pesa hizo ni za kuwapatia Wajumbe.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameandika ujumbe @Twitter kukanusha kuhusika na mtu huyo

  • “Kuna taarifa za uongo zinazoenezwa kwamba kuna “Mtu wa Membe” amekamatwa na pesa Dodoma“


Kwenye Tweet nyingine Waziri Membe ameandika hivi

  • ”siasa hizi ni za hovyo kwani hazitajenga Taifa letu. Naomba msihadaike na watu wanaotaka kututia doa baada ya kukosa uchafu dhidi yetu”  @BernardMembe

Akamatwa na Mamilioni Akitaka kuwa Onga Wajumbe wa Halmashauru Kuu Dodoma

Mtu mmoja amekamatwa mkoani dodoma na maburungutu ya fedha hotelini, inasemekana alikuwa na lengo la kuwahonga wajumbe wampitishe mmoja wa gombea uteuzi..nani kamtuma???
Updates Kutoka Jamii Forums:

Hapa St. Gasper Hotel ambapo ilikuwa ni kambi ya Edward Lowassa sasa hivi zimekamatwa fedha zinazodaiwa kuandaliwa kugawiwa kwa wajumbe wa NEC.

Aliyekamatwa kageuka, anasema katumwa na Membe

Mpasuko CCM: Wajumbe Waanzisha Varangati........Rais Kikwete Apokelewa Kwa Wimbo Wa Tuna Imani Na Lowassa.....!!!!.....Tuna Imani na Lowassa

Mambo yamezua jambo ambapo wajumbe wa mkutano wa Halmashauri kuu inayokutana hivisasa chini Rais Dkt Jakaya Kikwete wameonesha wazi kupinga uamuzi wa mbunge wa Monduli Edward Lowassa jina lake kukatwa.

Hayo yamedhihirika hivisasa wakati Mwenyekiti wa chama hicho Rais Dkt Jakaya Kikwete akiingia kufungua mkutano huo ambapo imezoeleka wajumbe huimba kuwa na imani na Mwenyekiti ambaye ni Rais Dkt Jakaya Kikwete lakini leo hali imekuwa tofauti.  Wajumbe walipaza sauti zao wakiimba wimbo wa kuwa na imani na Edward Lowassa.(  Tuna  Imani  na  Lowassa...!!!  Tuna  Imani  na  Lowassa!!)

Mkutano huo  wenye wajumbe  324 kati ya 374 umehudhuriwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo baadhi ya wanasiasa walio omba ridhaa ya kuteuliwa kugombea urais ndani ya chama hicho.

Kwa upande  mwingine  mtia nia aliyechujwa Prof. Mark Mwandosya yeye kwa upande wake amewashukuru wananchi kwa ushirikiano walio mpa na kusisitiza kuwa hatogombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.