Nani ambaye alikuwa hayajui mahusiano ya Wema Sepetu na Diamond? Hakuna ila yalikuja yakazima ghafla kama mwanga wa mshumaa, kila mtu akaendelea na maisha yake lakini vita ya mashabiki wao haijaisha kiasi cha wao wenyewe kushindwa hata kupeana support.
Hali hiyo imemchosha mwanadada, Wema Sepetu ambaye ameamua kutoa ya moyoni, amesema anatamani kuonana na Diamond wazungumze wamalize tofauti zao.
“Na nnatamani, one day tuweze hata tuka kaa hivi tukaongea nikamwambia bwana embu tuondokane na mambo haya yote whatever it is me nitakusupport, wewe ukinisupport wala usiponisupport sababu yule naye mswahili sana” Wema Sepetu alifunguka
Mbali ya kutaka kuyamaliza Wema amefunguka kuwa bado kuna kutoka kwa Diamond ambaye amedai kuwa bado anampinga kwenye mambo mengi, ametolea mfano jinsi Diamond alivyotaka kufanya kumpokonya ukumbi wa King Solomon kwa kutaka kulipia siku moja ambayo na yeye amepanga kufanya show kwenye ukumbi huo,
“Me naandaa hii show ya Christian Bella, nimepata ukumbi pale King Solomon sawa, yule mtu wa King solomon nimefika pale, tumeshaongea bei ya ukumbi na kila kitu nikamwambia mimi hapa nitakuja kulipa jumangapi jumatatu, tumeongea ilikuwa Ijumaa, Jumamosi naongea na yule mtu wa King Solomon, Jumatatu naenda pale naambiwa hivi, naambiwa kwamba Diamond anataka kuuchukua ukumbi kwa tarehe hiyohiyo tisa unaona, nikamwambia hivi, nikamwambia hivi ye anataka ku’host party? akanambia nimemwambia ukumbi umechukuliwa akaniuliza na nani, nikamwambia kachukua Wema, akanambia me niko tayari kupanda dau, Unaona” Wema aliendelea kuelezea “Mwisho wa siku me namchukulia Diamond kama mtu ambaye amekuwa kimuziki lakini yeye ki’personality bado”
Hata hivyo Wema amesema kwasasa hawezi tena kurudiana na Diamond, amedai kuwa kwasasa anamuona kama icon wa muziki wa Bongo tu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)