Sugu anadaiwa kufanya kitendo hicho June 6, mwaka huu alipokuwa akitoka katika ukumbi wa Bunge baada ya kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani kuhusu azimio la bunge kuridhia mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni.
Naibu Spika ameitaka kamati hiyo kumchukulia hatua kali kama watamkuta na hatia ya kufanya kitendo hicho