Serikali ya Tanzania ijibu tuhuma nzito za serikali ya Kenya, rais Magufuli asaidiwe kidiplomasia


Serikali ya Tanzania sasa itoke hadharani kujibu Tuhuma za Serikali ya Kenya na viongozi wa Muungano wa JUBILEE kuwa Rais Magufuli anamdhamini kifedha Kiongozi wa Upinzani Raila Amolo Odinga kusababisha Maandamano, ghasia na hatimaye kuipindua serikali ya Rais Uhuru Kenyatta.

Siku Chache Zilizopita Msemaji wa Serikali ya Kenya Erick Kiraithe alisema kuwa tayari kuna taarifa za kijasusi kuwa kuna wanasiasa nchini Kenya wanadhaminiwa na kusaidiwa na Nchi Mbili Jirani maadui wa Kenya kutaka kuvuruga amani na kuiangusha Serikali na kudai kuwa Baraza la Ushauri la Usalama (National Security Advisory Council) lilikutana siku ya Jumatatu kuangalia namna ya kuwashughulikia watu hao

Mbunge wa Jimbo la Starehe Mwenye ushawishi ndani ya Serikali ya JUBILEE akiambatana na wabunge wengine alifanya mkutano na waandishi wa Habari Nairobi Hoteli na Kuwataja marais John Magufuli wa Tanzania na Salva Kiir wa Sudan ya Kusini

Rais Magufuli akiwa mapumzikoni CHATO msimu wa Sikukuu ya Pasaka alikua Mwenyeji wa Raila Odinga anayejiandaa na Uchaguzi nchini Kenya mwaka 2017

Pia Mwezi Desemba nilialikwa na Mwenyekiti wa Vijana wa ODM wakati huo Rashid Mohammed n kwenye mkutano mkuu wa chama cha ODM kumteua Mgombea Urais 2012 nchini Kenya.Mhe.Magufuli pia alikuwepo. Nilimshuhudia Mhe.Magufuli akiwa waziri wakati huo akidai amehudhuria mkutano ule na kutangaza kuwa Raila Odinga ni Rafiki yake na amekuja kumuunga Mkono.Aliendelea kushtua watu Ukumbini akidai kwamba wagombea wengine wanaotarajia kuchuana na Raila Odinga hawawezi kusafiri hata nje ya nchi.Kipindi Hicho Uhuru Kenyatta na Willium Ruto walikuwa wanakabiliwa na mashtaka mahakama ya kimataifa ya ICC.

Mhe.Magufuli akaendelea kusema hata Odinga angegombea jimbo la Chato yeye Magufuli asingethubutu kugombea maana asingeweza kumshinda

Urafiki binafsi wa Raila Odinga na Rais Magufuli sio tatizo jwani hata Mwalimu Nyerere alikua na urafiki na akina Thom Mboya,Jaramogi Oginga Odinga ila tatizo ni pale ambapo Mhe.Magufuli anaposhindwa kuwa senstive kisiasa na Kidiplomasia.Mbaya zaidi tuhuma zinatolewa na serikali ya nchi jirani tena mwanachama ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa Rais Magufuli anatumia Raslimali za nchi kumfadhili Mpinzani wa nchi jirani kwa lengo la kupindua serikali kwa sababu ya urafiki wao tu

Nikumbushie tu kitendo alichofanya Mhe.Magufuli kipindi kile nilisema na niliandika kuwa kitakuja kuleta matatizo ya kidiplomasia siku za usoni ikiwa ODM wangeshindwa kwani tayari kupitia Udhaifu alioonyesha waziri wa serikali ya Tanzania Mhe.Magufuli wakati Ule walishaaminisha Umma kuwa serikali ya Tanzania inawaunga Mkono.Kosa hili la Kidiplomasia ameendelea kulirudia.

Rais Jakaya Kikwete alikuwa Rafiki wa Kalonzo Musyoka lakini Uhusiano wao haujawahi kuibua mgogoro wa kidiplomasia na au kutoaminiana baina ya serikali hizi mbili

Tuhuma hizi ni nzito na zinazochochea mgawanyiko ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Kitendo cha Serikali ya Tanzania kukaa kimya hadi muda huu maana yake kinatoa Silent Consent kuwa nu kweli hasa msemaji wa Serikali anaposema kwa ujasiri kuwa serikali yao ina taarifa rasmi

Mwaka 2013 kulikua na mgogoro wa kidiplomasia uliotishia kuipasua Jumuiya ya Afrika Mashariki .Kenya,Uganda na Rwanda ziliunda Muungano wao wa hiyari (Coalition of The Willing-CoW).Jitihada kubwa za kidiplomasia zilifanyika

Sasa muda huu Rais Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Africa Mashariki na Tanzania kama Mwenyekiti hatupaswi kuwa chanzo cha migogoro ndani ya jumuiya kwani sisi ndio tunaopaswa kuonyesha uongozi katika Diplomasia kuhakikisha Malengo ya Mtangamano(Intergration) yanafikiwa.

Jitihada zozote za Serikali ya Tanzania na wapambe wake kutumia propaganda pengine kwa kuibua hoja ya Bomba la mafuta Kutoka Uganda na Kupita Tanzania badala ya Kenya na Suala la Reli ya Rwanda kwamba ndio limesababisha wivu itakua ni uamuzi mbaya kidiplomasia

Serikali ya Tanzania ijibu tuhuma hizi kama si kweli basi Serikali ya Kenya iombe Radhi

Kenya na Tanzania zinahitajiana kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote kiuchumi

Katika tathmini iliyotolewa bungeni jana,biashara ya Kenya na Tanzania imechangia sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi hizi

Mawaziri wa Mambo ya Nje ambao ni wanadiplomasia Maahiri Dr.Augustine Mahiga wa Tanzania na Amina Mohammed Jibril wa Kenya wasaidie kunusuru hali hii ambayo inahatarisha Uhusiano wa Kidiplomasia baina ya Nchi hizi Mbili

Na Pia Rais Magufuli asaidiwe ili apate uzoefu wa Kidiplomasia katika maneno na matendo yake.

Kwa mfano kitendo cha kuongea na Rais Kenyatta mwezi March walipokutana Arusha na kuahidi kusaidiana kuondoa vikwazo vya kibiashara baina ya nchi hizi mbili na kisha mwezi mmoja baadae kumwalika Raila Odinga akiwa Mapumzikoni(Inaweza kutafsiriwa alichukua likizo ili akutane na Odinga isionekane amekutana nae ikulu) hakikutoa gesture nzuri kidiplomasia

Wakati Rais Magufuli anahutubia mkutano wa mfuko wa Wafanyabiashara Mwezi Desemba 2015 aliitaja kampuni ya Broakside Dairy Limited kuwa ilikua ikifanya biashara kiadui na kinyume na misingi ya Biashara nchini.Kampuni hiyo ilimilikiwa na familia ya Rais Uhuru Kenyatta.Kidiplomasia Rais hakupaswa kutamka na kuitaja kamapuni ile bali angeweza kukwepa na kutumia namna nyingine au mtu mwingine kama ilikua ni lazima itamkwe.Siitetei kampuni ile isipokua ni udhaifu mkubwa wa kidiplomasia aliouonyesha Rais ingawa anaweza kujitetea kuwa alikua anasimamia Sheria.Diplomasia ni namna ya kumwambia mtu kafie mbali na yeye akakuuliza mbali kiasi gani badala ya kukukasirikia.Rais anapaswa ajifunze hili

Sasa hizi tuhuma za serikali ya Kenya na viongozi waandamizi zijibiwe na kama si kweli serikali ya Kenya Iombe Radhi.

Kama ni kweli inawezenaje Wanachi wa Tanzania wakose Sukari halafu Rais afadhali shughuli kama hizo nchi jirani?Na iweje sasa Serikali yake izuie mikutano ya kisiasa nchini?

Aluta Continua,Victory Ascerta......

Ben Saanane