Kitendo cha Watu Kumchangia Pesa Aliyemtukana Rais Chafika Bungeni...Mbunge Adai ni Dharau Kwa Taifa



June 21 2016 Mbunge wa Nchemba Juma Nkamia alisimama bungeni kuomba mwongozo wa bunge kujadili tukio la mtuhumiwa wa kesi ya kumtukana Rais Magufuli kuchangiwa fedha na watu kwa ajili kulipa fidia, kitendo kinachoashiria dharau. Mwongozo wa Nkamia ukaungwa mkono pia na Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde.

Nkamia alisema…
’Kuna mtu alimtukana Rais na akahukumiwa kwenda jela au kulipa faini ya milioni 7, alilipa nusu ya faini ile na akaruhusiwa aondoke akatafute fedha nyingine. Nilitaka wanasheri watusaidie, hivi kumtukana Rais wa nchi alafu yule aliyetukana anaruhusiwa akatafute fedha za kulipa‘ –Juma Nkamia

‘Siku ya kukabidhiwa fedha anaita na waandishi wa habari, na baadhi ya wabunge humu ndani wa chama fulani walionyesha wananchangia fedha yule mtu ili akalipe faini. Kwahiyo ni maana kuwa alitumwa na chama hicho akamtukane Rais.’ –Juma Nkamia

‘Sasa naomba kujua sio dharau kwa Rais? sheria inaruhusu jambo hili kufanyika? na kama mimi leo nikahukumiwa kwa kesi ya kuiba kuku siwezi kuruhusiwa kutafuta fedha, iweje mtu huyu akaruhusiwa kutoka nje kutafuta fedha na bado akaonekana watu wakimkabidhi fedha? hizi ni dharau kwa taifa kwa ujumla‘ –Juma Nkamia