Kidoa: Nimemisi kutukanwa, kuvaa kihasara!


Video Queen mwenye figa matata, Asha Salum ‘Kidoa’ amefunguka kuwa, ndani ya mwezi mtukufu amemisi kufanya na kufanyiwa mambo kibao ikiwemo kuvaa nusu utupu na kutukanwa mitandaoni.
Kidoa aliitonya safu hii kuwa kabla ya mwezi mtukufu alikuwa huru kupiga picha za mapozi na kuvaa anavyotaka kisha kutupia mitandaoni lakini sasa hivi anabanwa kufanya hivyo.

“Ukiacha hilo la kuvaa mavazi yangu yale niliyozoea, pia nimemisi kutukanwa, si unajua nilipokuwa nikitupia picha hizo wapo watu waliokuwa wakinitukana. Huwa siogopi hilo, nimezoea na ninaona ni kama sehemu ya maisha yangu,” alisema Kidoa.