Leicester imesema kuwa mchezaji huyo wa miaka 29 ambaye mabao yake yameisaidia klabu hiyo kushinda taji la ligi ya Uingereza msimu uliopita ameongeza mkataba wa miaka minne na klabu hiyo.
Aidha, uamuzi wa mchezaji huyo utafuta uvumi wa hivi karibuni kuhusu Jamie Vardy kuachana na klabu hiyo na kwenda Arsenal.
Vardy alitarajiwa kununuliwa na klabu ya Arsenal kwa kitita cha pauni milioni 20 kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro 2016.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)