Ameandika Josephine Mshumbushi mke wa Dr.W.Slaa katika ukurasa wake rasmi wa Facebook
Kwa Vijana wa CHADEMA!
Salaam,
Miaka 15,iliyopita sikuwahi kujua watoto wangu wataishi kuyasoma maandiko yangu nakunihoji au kuniuliza maswali.
Leo hii inatokea.
Ngoja niweke kumbukumbu sahihi!!!!
Kitendo cha kuwaita watu wasaliti ni kwakuwa mtu umeshindwa hoja ya kumshawishi akubaliane na wewe.
(Don't let personal hangups sidetrack the negotiations)
Na hili ndilo limekuwa anguko la CHADEMA toka nilipokijua chama hicho!
Mawazo au maamuzi ya mtu hayahojiwi.
Kwanini unaitwa mtu mzima!!!!!
Ni kwa kigezo kwamba sasa unaweza kufanya maamuzi yako bila shinikizo.
Maamuzi ya mtu lazima yaheshimiwe japo mengine yamekuwa magumu kuyakubali.
"In one of my job interview I was asked,how do you feel when you are asked to fire somebody"
.........very sad,however decisions have to be made for things to move foward."
Ninyi Vijana Hakuna anayeijua CHADEMA, tena Leo ambapo kila mtu ni msemaji.
Anayeijua CHADEMA ni mtu mmoja tu, aliyebeba maono na kukianzisha (Mzee Mtei)
"what the transitions follows non of my business.........."
Mimi na wewe ni .................
Ndiyo maana ndani ya CHADEMA mtu mmoja tu anaweza kuuwa chama.........
Tofauti na CCM.
Mwl hakuianzisha TANU kama taasisi, Bali lilikuwa ni kundi kubwa la watu, na likamchagua kama kiongozi kwa kuwa he has a commanding power element.
Heshima na nidhamu iliendelea kujengwa mpaka Leo kwa viongozi wote.
Huwezi na Hakuna maandiko ya mtu kuitwa msaliti ndani ya CCM. Kwakuwa ni kundi kubwa lililojengwa kwa hulka ya kuheshimu mawazo ya mtu na kuyapa mda yapite.
CHADEMA kimejengwa kwa nidhamu ya woga.Ndiyo Maana wengi waliamini kwa kujiweka karibu na wakubwa ndiyo fursa yao yakuonekana na kufikia malengo.
Mfano kila mtu anafanya jambo awe recognized na Mbowe na enzi hizo na Dr Slaa pia.
Tabia hii imeendelea kuzaa majungu na hofu ya kutojiamini.
Watu wenye mawazo Yao wameshindwa kuyatoa kwa kuhofu kutosikilizwa.
Lakini hata wale wenye mtazamo tofauti wameshindwa kuisimamia wasipoteze nafasi zao.
(Haya yanaishi ndani ya vijana wengi leo)
Ndiyo maana tunaona post nyingi leo ili mradi mtu kaandika kitu. Mbaya zaidi Hakuna mwongozo wa Nini kiandikwe wapi na kwa wakati gani.
Hivyo maamuzi tuliyofanya.
1.We trusted on our strengh.
2.We wanted to end relationship with the problem.
Enyi wafia chama ni vema mkatambua hamjai hata kwenye kiatu changu, nimetengeneza historia yangu, na bado naitengeneza historia yangu.
Yote mnayofanya yanapita ila kitendo cha kumkataa mtu tuliyemuita fisadi kitadumu Milele.
And that is our strength .