Blac Chyna ametaja sababu za kukubali kuwa mama

Mwanamitindo mwenye skendo nyingi Angela White ‘Blac Chyna’, 28, hivi karibuni amefunguka juu ya sababu za kwa nini anahitaji kumzalia mtoto mchumba wake Rob Kardashian mwenye miaka 29.

Akipiga stori na mtandao fulani wa burudani Marekani, mwanadada huyo ambaye pia ni mzazi mwenza na Tyga kwa mtoto wao wa kiume King Cairo Stevenson alisema yuko tayari kumzalia Rob kwa sababu anafikiri ni aina ya baba bora na mtu ambaye anafahamu juu ya majukumu yake.
“Nampenda sana Rob, nafikiri ni wakati muafaka wa kumzalia mtoto kwa sababu ni aina ya baba bora na anafahamu jinsi ya kutimiza majukumu yake kama kichwa cha familia,” alimaliza Blac.