Jack Wolper:Sijawahi Lia eti Nimeachwa Nikamwaga Chozi Sababu ya Mwanaume

STAA wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa tangu aanze kujihusisha na masuala ya mapenzi hajawahi kulia.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper ambaye ana muonekano wa ‘kigumu’, alisema siku zote anaamini katika kupambana hivyo hawezi kumlilia mwanaume hata iweje.

“Sijawahi kulia pale nilipoachwa wala kuachana na mwanaume, akili yangu yote inaamini katika kutafuta maisha hivyo siwezi kujirahisisha nikamwaga machozi kwa ishu za mapenzi,” alisema Wolper