NEC: Hatutaahirisha Uchaguzi Mkuu Oktoba, wala Kuiongezea Muda Serikali iliyopo Madarakani

Tume ya uchaguzi nchini (NEC)imesema tarehe ya Uchaguzi mkuu Mwaka huu iko pale pale  ambapo ni siku ya terehe 25 mwezi octoba mwaka huu.

Kauli ya NEC inakuja ikiwa ni siku moja kupita baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe kuitangazi serikali kiama endapo itasogeza mbele tarehe ya uchaguzi mkuu

Akifanunua Kauli hiyo ya Mbowe leo Jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa NEC Jaji mstaafu Damian Lubuva wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari amesema taarifa zinazosemwa na wanasiasa kwamba tume hiyo itasogeza mbele uchaguzi Mkuu  si za kweli na  zinalengo la kuwachanganya wananchi kwani tume hiyo inakwenda vizuri na uandikishaji wa Mfumo mpya wa BVR.

Jaji Damian ameongeza kuwa kwa sasa Uandikishaji wa Wapiga kura kwenye Mkoa wa mdogo wa Njombe unatarajia kumalizika kesho na kuanza rasmi uandikishaji kwenye mikoa mingine ya Mtwara,Lindi na Iringa ambapo amasema kwa sasa watafanya kwa kasi zaidi.

Amebainisha kuwa tatizo lililokuwa linawakabili kwa kuwa na mashine chache za uandikishaji wamelitatua kwakuwa sahivi tayari mashine nyingine 1600 zinatarajiwa kuwasili  kesho, jambo ambalo anadai litafanikishwa kasi ya uandikishaji.

Aidha,amesema shehena nyingine ya mashine inatarajiwa kuja tarehe 25 mwezi huu na mpaka ifikapo mwezi wa Sita mwaka huu watakuwa wameshapata mashine zote elfu nane walizokuwa wakizihitaji , jambo ambalo amesema litawafanya wamalize kuwaandisha wananchi nchi nzima  mwezi wa saba mwaka huu. A