Floyd Mayweather amemdunda Manny Pacquiao kwa points baada ya pambano la dunia lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kumalizika huko jijini Las Vegas.

Pacquiao kama ilivyokuwa ikitarajiwa alirusha ngumi nyingi zaidi kuliko mpinzani wake lakini Mayweather aliweza kurusha ngumu zenye faida zaidi zilizowafanya majaji wanne wampe ushindi.
Mayweather ameshinda kwa point 118-110, 116-112, 116-112. Kwa ushindi huo, Mayweather ameendelea kushikiliza rekodi yake ya kutowahi kushindwa katika mapambano yake 48 aliyowahi kupigana.
Tazama picha za pambano hilo.










