Showing posts with label VIDEO. Show all posts
Showing posts with label VIDEO. Show all posts

Kitendo cha Watu Kumchangia Pesa Aliyemtukana Rais Chafika Bungeni...Mbunge Adai ni Dharau Kwa Taifa



June 21 2016 Mbunge wa Nchemba Juma Nkamia alisimama bungeni kuomba mwongozo wa bunge kujadili tukio la mtuhumiwa wa kesi ya kumtukana Rais Magufuli kuchangiwa fedha na watu kwa ajili kulipa fidia, kitendo kinachoashiria dharau. Mwongozo wa Nkamia ukaungwa mkono pia na Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde.

Nkamia alisema…
’Kuna mtu alimtukana Rais na akahukumiwa kwenda jela au kulipa faini ya milioni 7, alilipa nusu ya faini ile na akaruhusiwa aondoke akatafute fedha nyingine. Nilitaka wanasheri watusaidie, hivi kumtukana Rais wa nchi alafu yule aliyetukana anaruhusiwa akatafute fedha za kulipa‘ –Juma Nkamia

‘Siku ya kukabidhiwa fedha anaita na waandishi wa habari, na baadhi ya wabunge humu ndani wa chama fulani walionyesha wananchangia fedha yule mtu ili akalipe faini. Kwahiyo ni maana kuwa alitumwa na chama hicho akamtukane Rais.’ –Juma Nkamia

‘Sasa naomba kujua sio dharau kwa Rais? sheria inaruhusu jambo hili kufanyika? na kama mimi leo nikahukumiwa kwa kesi ya kuiba kuku siwezi kuruhusiwa kutafuta fedha, iweje mtu huyu akaruhusiwa kutoka nje kutafuta fedha na bado akaonekana watu wakimkabidhi fedha? hizi ni dharau kwa taifa kwa ujumla‘ –Juma Nkamia

Familia Yaingilia ishu ya Mwanaume Shoga Kumtaka Mwanamuziki Juma Jux...

 Familia ya staa wa Bongo Fleva, Juma Musa ‘Jux’ imeingilia kati ishu ya mwanaume ‘tata’, mkazi wa Dar, James Delicious aliyetangaza kumtaka kimapenzi msanii huyo ambaye ni mpenzi wa Mwanamuziki Vanessa Mdee ‘V-Money’.

Akizungumza na Wikienda kwa niaba ya familia, dada wa Jux, Fatu-ma Juma alisema kuwa hakuna kitu kinachowaudhi kama kijana huyo kutwa kutangaza kumpenda na kumtaka mdogo wao huyo wakati wote ni wanaume na ni kinyume cha maadili ya kidini (familia ya Kiislam), Kitanzania na Kiafrika kwa jumla.

“Kiukweli familia inachukizwa sana na tabia ya huyo kijana ambaye haoni aibu, tunamtaka kuacha mara moja kusumbua watu akitaka namba ya Jux la sivyo tutachukua hatua za kisheria kwani anatukera sana,” alisema Fatuma.

Hivi karibuni kijana huyo alitangaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa lazima ampindue Vanessa kwa Jux kwani anampenda jamaa huyo kupita kiasi.

ANGALIA UNYAMAAA ALIOFANYA JAY MOE KWENYE VIDEO YAKE MPYA #PESA YA MADAFU,


BONGO CREW RATINGS:
Sound:10/10
Picture quality:10/10
Acting:9/10
Story board:10/10


VIDEO:Young D Akwidwa, Atiwa Mbaroni..Kisa Kizima Hichi Hapa..

Kimemnukia! Mbongo Fleva, David Genzi ‘Young D’ amejikuta mikononi mwa askari wa Kituo cha Polisi Urafiki, Ubungo jijini Dar madai yakiwa kuharibu simu na kushambulia mwili, Amani lina kila kitu.

Ilidaiwa kuwa, katika siku za karibuni, msanii huyo alimshambulia mrembo aliyejulikana kwa jina moja la Nasra lakini pia aliharibu simu yake yenye thamani ya shilingi 600,000.
Juni 6, mwaka huu, yaani Jumatatu iliyopita, Young D akiwa nyumbani kwake, Sinza Mori jijini hapa, aligongewa mlango na kutakiwa kutoka.

“Lakini alipotoka na kugundua ni askari na wanamtaka waende naye kituoni, alileta ujeuri kidogo, ikabidi wamkwide na kumuweka chini ya ulinzi mpaka kituoni.
“Mbaya zaidi, alikuwa hajavaa shati ni suruali tu, ikabidi aende polisi hivyohivyo. Unajua hawa wasanii wetu bwana sijui huwa wanawaza kitu gani katika ustaa wao,” kilisema chanzo kimoja kilichoshuhudia dogo huyo akiwekwa mtu kati na askari hao.


Habari zaidi zinasema kuwa, Nasra na Young D ni wapangaji wa nyumba moja lakini hawana uhusiano mzuri kwani mara kwa mara wamekuwa wakikwaruzana kwa sababu ambazo hazijulikani kirahisi.

“Siku ya tukio, inasadikiwa kuwa walikwaruzana sana, ndipo dogo (Young D) akaamua kumvaa mwanadada huyo na kumpa vitasa (ngumi) kisha kuivunja simu yake,” kiliongeza chanzo.

Katika Wabongo Fleva wanaotamba, Young D naye yumo ambapo amepata jina kupitia vibao vyake viwili, Ujanjaujanja na Kijukuu.

Askari mmoja wa Kituo cha Urafiki ambaye aliomba asiandikwe jina kwa sababu si msemaji, alipoulizwa na Amani kuhusu hatima ya mwimbaji huyo alisema: “Upelelezi unaendelea, ukikamilika atapelekwa mahakamani.”

VIDEO:Jionee Wizi Mpya wa Mpesa na Tigo pesa, Jamaa Kaibiwa Sh 720,000

Utapeli umekua mwingi sana hapa mjini, watu wengi wanatapeliwa kila siku. Kutapeliwa ni kutapeliwa tu haijalishi ujanja utakaotumika ni wa sasa au wa zamani. Ila siku za karibuni kumetokea aina mpya ya utapeli ambao wahathirika wakubwa ni watu wanaotoa huduma za Mpesa na Tigo Pesa.

Kama utakavyoona katika video hii ni ngumu sana kugundua kama umeshatapeliwa mpaka baada ya mdaya mda upite. Kwa mfano huyu jamaa aliyetapeliwa hapa kaibiwa 723,000 na matapeli hao. Hebu tazama video hii na wewe usije ukaibiwa kama huyu.