Showing posts with label SKENDO. Show all posts
Showing posts with label SKENDO. Show all posts

NI SHIDAAA,MBAVU ZANGU JAMANII!!

 Hhaha, inachekesha sana jamani....hawa ni watoto wa familia moja ya kipekee sana duniani!! Inawezekana kabis a wakawa wameingia kwenye maajabu saba ya dunia. Kuna mmoja huyo anayekuangalia anatafuta mke, anataka kuja KUKUTOLEA POSA WEWE UNAYESOMA HII HABARI. Teh teh teh.....Samahani natania haha

MKE WA MTU AFUMANIWA AKILIWA URODA NA HOUSE BOY...INSHU YOTE IKO HAPA

Zamani tulikuwa na hofu na mahouse girl kuvunja ndoa za watu lakini kwa sasa mabo yamebadilika.Kiongozi mkubwa mstaafu serikalini (Mr Kelechi) ameshangazwa na kile kinachoitwa sintofahamu baada ya kuona maajabu kwenye simu ya mfanyakazi wake wa 
kiume 
wa nyumbani kwake(house boy).
Taarifa zinasema kiongozi huyo alichukua simu ya mfanyakazi wake iliafanye mawasiliano lakini katika kuichezea alizikuta picha za uchi za mke wake.Mapigo ya moyo yalibadilika, ndugu msomaji usiombe uibiwe mke ni bora ukaibiwa hata pesa.

MAAJABU:MWANASHERIA AISHITAKI ISRAEL KWA KIFO CHA YESU

Maajabu mengi sana hugundulika duniani kila siku , lakini kuna kila uwezekano kuwa ajabu lililoko kwenye story hii likawa ajabu la kipekee . Mwanasheria mmoja ambaye ni raia wa Kenya ameibuka na kuzishitaki serikali za Israel na Italia kwa kosa la kuhusika kwenye kifo cha Yesu Kristo .
Mwanasheria huyo Dola Indidis amefungua kesi hiyo kwenye mahakama ya dunia The Hague kule kule ambako rais wa taifa Lake (Kenya ) Mh Uhuru Kenyatta na Makamau wake William Ruto nao wana kesi ya kujibu .
Mwanasheria huyo amesema kuwa lazima serikali za mataifa hayo ziwajibike kwa kitendo cha unyama alichofanyiwa mwanzilishi wa dini ya madhehebu ya Kikristo ambaye ni Yesu aliyesulubiwa msalabani pasipo kuwa na hatia yoyote ya kustahili adhabu hiyo . 
Dola Indidis amefungua shitaka hilo dhidi ya Mfalme wa uliokuwa Ufalme wa Roma Tiberio pamoja na watawala waliokuwa chini yake wakati huo wakiwemo Pontio Pilato na Mfalme Herode pamoja na viongozi wa kiyahudi wakiwemo mafarisayo na masadukayo ambayo kwa pamoja walikula njama ya kumuua Bwana Yesu .

Indidis anasema kuwa ushahidi uko kwenye kitabu kitakatifu Cha Biblia ambayo kila mmoja anafahamu kuwa haisemi uongo . Kwa kuwa wafalme na watawala waliohusika na kitendo hicho hawako hai serikali ambazo mipaka yake ndio ile ile ya iliyokuwa falme ya Roma iliyokuwa madarakani kipindi hicho zitawajibika kwa niaba .
Dola Indidis anasema kuwa vitendo alivyofanyiwa Yesu ni vitendo vya kinyama na ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nay eye kama mwanadamu anahisi kuwa ni jukumu lake kulinda na kutetea heshima ya Yesu Kristo.

Hata hivyo msemaji wa mahakama ya Dunia ambaye hakutajwa utambulisho wake amesema kuwa hakuna kipengele cha kisheria ambacho kinaweza kuruhusu kusikilizwa kwa kesi hiyo kwani ICJ (International Court Of Justice) husikiliza kesi zinazohusu nchi dhidi ya nchi nyingine hivyo kesi hiyo haiwezi hata kufikiriwa . Indidis kwa upande wake bado ana imani kuwa ana kesi ya kuhoji na anaamini kuwa atashinda kesi hiyo.