Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Ngemela Lubinga amekanusha taarifa za kuibiwa kwa kifaru cha jeshi hilo ambapo amekana juu ya taarifa hiyo na kusema kuwa hazina ukweli.
Kanali Ngemela Lubinga amesisitiza kuwa, JWTZ lipo imara katika ulinzi kwa maeneo yote ya nchi. Hata hivyo Jeshi hilo limeitaka Gazeti hilo lililoandika habari hizo liombe msamaha kwa taarifa yake hiyo kwani jeshi hilo limekuwa ni mkombozi wa Nchi nyingi za Afrika na limekuwa mstari wa mbele katika masuala ya Amani, hivyo kwa taarifa kama hiyo inaleta taswira mbaya kwa Mataifa mengine.
Tazama MO tv, kuona tamko hilo la JWTZ hapa:
Awali leo Juni 20.2016 kumeibuka mijadala kwenye mitandao ya kijamii juu ya gazeti hilo la kila siku kuandika habari juu ya kuibiwa kwa kifaru cha jeshi, huku watu/wananchi wakiipokea kwa hisia tofauti za kuibiwa huko.