MAKAHABA WANASWA WAKIPIGANA ' UCHI ' MAKABURINI!!!

 
Habari hii inayoonekana ya kuchekesha inahusisha mkasa mzito uliotoke hivi karibuni ambapo Machangudoa wawili walikamatwa na Jeshi la POLISI kwa shutuma  za kupigana katika maeneo ya maziko kinyume na sheria.
 
Taarifa zaidi zinadai kuwa akina dada hao wakekuwa MASHOSTI kwa muda mrefu hivi sasa na kitendo wao kupigana katika eneo nyeti kama Lile ni aibu sana. "Mara nyingi wamekuwa wakionekana wanatembea pamoja kitu kinachoashiria kuwa walikuwa ni marafiki wa muda mrefu sana, Lakini tunashanga leo kuwaona wanapigana hapa " Alisema shahidi ambaye alikuwepo eneo la tukio.
 
Baada ya kukamatwa na kuhojiwa makahaba hao walishutumiana na kurushiana maneno machafu huku kila mmoja akidai kuwa ameibiwa bwana wake. "Nilikuwa nasikia muda mrefu kwmba anatembea na bwana wangu na juzi nimemkuta baa anakunywa nae, kwahiyo leo nimeamua nimkomeshe" alidai mmoja kati ya makahaba hao.
 
Vitendo vya UKAHABA vimekuwa gumzo hivi sasa Barani Africa kwani Takwimu zinabainisha kuwa Idadi kubwa ya wanawake ambao wanashindwa kuendelea na masomo kwa sababu moja ama nyingine basi hujiingiza katika biashara hiyo muhimu ya kuuza miili yao.