Lulu Afuata Nyayo za Wema, Ahamasisha Matumizi Bora ya Mitandao ya Kijamii

Staa mrembo kutoka Bongo movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ mwenye followers zaidi ya laki nne kwenye mtandao wa Instagram amewataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kujengana zaidi ikiwa ni siku chake baada ya staa mwenzake, Wema Sepetu kuwataka wanawake na jamii kwa ujumla kutumia mitando hiyo kuhamasishana kwenye vitu vya kimaendeleo zaidi.

“Nikiwa kama kijana mpenda maendeleo,mwenye ndoto na malengo ya kufika mbali najua mawazo yangu pekeyangu yanaweza yasitoshe mimi kufika ninapopataka….najua wapo vijana wengi wenye nia kama yangu..!
Nadhani umefika wakati wa kutumia mitandao ya kijamii kwa kujengana na kusaidiana hasa ki mawazo ili wote tuweze kuwa sehemu flani siku moja…..” Lulu amendika

Nadhani Ujumbe umeeleweka.