Kundi Laandaliwa Kumzomea Benard Membe Tamasha la Pasaka


Mkurugenzi wa ‪‎Msama‬ Promotion, Alex Msama ametoa onyo kwa kikundi cha watu kilichojipanga kumzomea Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ‪‎Bernard‬ Membe atakayekuwa mgeni rasmi wa Tamasha la ‪‎Pasaka‬ linalotarajiwa kufanyika hii leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi jana, Msama alisema kuwa amepata taarifa kuhusu uwapo wa mashabiki wa mwanasiasa mmoja, ambao wamenunua tiketi nyingi kwa lengo la kuzomea