Hivi karibuni Tumesikia Video Mbali Mbali zikifungiwa na mamlaka husika kuchezwa kwenye Vituo vya TV hapa East Africa lakini cha kushangaza hizo hizo Video zilizofungiwa kwetu zinachezwa kwenye Vituo vikubwa vya kimataifa, Mfano mmoja wapo ni Video ya hivi karibuni ya kundi la Souti Soul ya wimbo unaitwa Nishike ilipigwa marufuku Kenya lakini cha ajabu inachezwa Channel O ya South Africa..Je Mamlaka Husika za Nchi zetu zimepitwa na wakati ?
Wakati huo huo kuna Swali nalojiuliza kila siku unakuta TV za Hapa ndani wanapiga nyimbo za nusu utupu za wanamuziki toka nje vizuri kabisa lakini za wasanii wa kwetu unakuta hata si za nusu uchi ila unakuta mdada kazungusha mauno kidogo tu eti Video inapigwa marufuku mbona hizo za kina Beyonce hamzizuiii?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)