VERA SIDIKA: MAKALIO YANGU MAKUBWA NDIO YALIYOSABABISHA HII VIDEO KUPIGWA MARUFUKU;ITAZAME HAPA!

 Yule msichana anaesadikika kusababisha video ya P-Unit "YOU GUY" kuzuiwa kuoneshwa na kituo cha Televisheni cha Citizen nchini Kenya, Vera Sidika (pichani) azungumzia sakata hili linaloendelea nchini humo.

Vera akilizungumzia suala zima, anasema, "Ina maana Citizen TV hawaoneshi video za Rihanna akiwa nusu uchi, wanaonesha video nyingi za aina hii kutoka ughaibuni ambazo si nzuri. Hata hivyo hiki ni kizazi kipya. Nilikuwa nimevaa gauni tu."

Vera alipoulizwa kuwa, anadhani video hii imezuiliwa kwa sababu yake, alijibu "Binafsi, sidhani kama kweli, labda ni kwa sababu ya mwili wangu ndo maana wanapindisha maneno, kama ingekuwa ni msichana mwembamba isingeonekana kuwa ni mbaya ila kwa sababu ya matako yangu, watu ndio wanachanganyikiwa na hilo"
Bonyeza Kusoma Zaidi:

Mapema mwaka huu, Citizen TV iliifungia video ya P-Unit inayojulikana kama "You Guy" kutokana na kuonekana kwenda kinyume na maadili. 
KAMA UNA HARAKA IRUSHE MPAKA DAKIKA YA 1:30 KUCHEKI MAMBO YA VERA SIDIKA!!!!