Mapya ya Gwajima yazidi kuibuka Dar, Bastola iliyokamatwa Juzi Gwajima Anaimiliki Kihalali


Mfano wa Bastola iliyokutwa
MAPYA yamezidi kuibuka katika sakata la Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Joseph Gwajima, baada ya kuthibitika kwamba bastola iliyokamatwa katika harakati za kile kinachotajwa kutaka kumtorosha kutoka katika Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam, ni mali yake.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema jana kuwa uchunguzi wa kina na wa kitaalam, sasa umethibitisha silaha hiyo inamilikiwa kihalali na Askofu Gwajima.

“Kuhusu risasi 17 za short gun ni kwamba Askofu Gwajima anamiliki bunduki aina ya short gun yenye namba 102837 ambayo inatumia risasi za aina ya hizo zilizokamatwa,” alisema Kamanda Kova.

Bastola hiyo ni moja ya vitu walivyokamatwa navyo wafuasi 15 wa Gwajima, wanaodaiwa kula njama za kutaka kumtorosha usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita.